News

 Home / News / News

Burkinafaso Wawazuia Wenyeji Gabon

Wenyeji Gabon, Jana walilazimika kutoka sare ya 1 kwa 1 na Burkinafaso. Hii ilikuwa baada ya Prejuce Nakoulma kuifungia Burkinafaso bao lao kupitia Mkwaju wa Penalti katika uwanja wa Stade de l’Amitie.

Mlinda lango wa Burkinafaso Hervé Koffi alionyesha umahiri wake katika mechi hii kwa kuokoa mashambulizi mengi yaliyoletwa na Gabon.

Pierre-Emerick Aubameyang aliweza kuifungia timu yake Gabon bao la kusawazisha. Mchezaji huyo wa kimataifa anayeichezea Borussia Dortmund alikosa nafasi zingine mbili katika mechi hiyo. sasa Gabon na Burkinafaso wanashikilia nafasi ya pili katika kundi la 'A' wakiwa na mabao 2 kila mmoja wao.

Gabon sasa watakuatana na Cameroon katika mechi ya mwisho ambapo Ushindi huenda usiwasaidie katika kuvuka kwa ajili ya kuenelea katika mashindano hayo.

Je, Gabon wataweza kufuzu kwa round nyingine ya Mechi hizi? Toa maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii.

Share on facebook

About Us

TV1 is part of the Modern Times Group (MTG), international presenters in entertainemt. MTG has operations in 4 continents. Visit www.mtg.se for more information.

Viasat 1 Tanzania Ltd.

  •   Mikocheni A Ind. Area, Plot No. 81,
         P. O. Box 31119, Dar es Salaam, Tanzania
  •   +255 658 455 121
  •   0 -000 -000 -0000
  •   info@tv1.co.tz

Email us

Your message was successfully sent!